emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Leseni za Uendeshaji

Ithibati za uendeshajiI wa shughuli za filamu

Wahusika ni wote wanaojishughulisha na kazi zozote za filamu na michezo ya kuigiza, matangazo, utayarishaji wa picha jongevu, miundombinu, studio,matamasha na tuzo za filamu.


Hatua za kupata leseni

  1. Kujaza fomu ya maombi
  2. Kuwasilisha fomu ikiwa na viambatisho vilivyoainishwa
  3. Kupatiwa leseni baada ya maombi kuridhiwa


Leseni, Ada na Vibali

    • Kumbi za sinema: TZS. 500,000 kwa mwaka
    • Maeneo ya uzalishaji kama studios: TZS. 200,000
    • Maeneo mengine: TZS. 36,000

Ada hii inalipwa kwa mwaka. Aidha tozo halisi hubainika baada ya uhakiki na ukaguzi wa taarifa za muombaji na/au miundombinu.

(Bonyeza hapa kupakua leseni za uendeshaji shughuli za filamu)

(Bonyeza hapa kupakua fomu ya maombi ya kitambulisho)