Habari
WARSHA YA KUTAFUTA MASOKO YA KAZI ZA FILAMU
Bodi ya Filamu Tanzania imeshiriki katika warsha ya kutafuta masoko ya kazi za Filamu iliyoandaliwa na Shirikisho la Filamu Uganda kwa kushirikiana na mdau wa Filamu nchini Prof. Martin Mhando.
Warsha hiyo ililenga kujadili namna bora ya kutengeneza soko la Filamu la pamoja kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika ufungaji wa warsha hiyo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Gervas Kasiga amewapongeza waandaaji kwa jitihada kubwa wanazozifanya ili kutafuta soko imara la filamu ndani ya Tanzania na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sambamba na hayo, Dkt. Kasiga amewahakikishia kuwa Serikali kupitia Bodi ya Filamu itaendelea kushirikiana na waratibu hao ili kufikia azma kunyanyua masoko ya filamu zetu.