emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Majukumu

Majukumu ya Bodi hii ni pamoja na:

 • Kuishauri Serikali kuhusu masuala ya filamu na michezo ya kuigiza nchini
 • Kusimamia na kuratibu maendeleo ya sekta ya filamu na michezo ya kuigiza nchini
 • Kupanga na kutoa madaraja ya viwango kwa wataalam na miundombinu: mfano watayarishaji, waigizaji, wasambazaji, wahariri, watafuta mandhari, waongozaji, wapiga picha, wasambazaji, studio, majumba ya uzalishaji wa filamu na maeneo ya uoneshaji
 • Kusimamia na kuratibu utengenezaji wa filamu na michezo ya kuigiza nchini
 • Kuandaa, kuratibu na kuendesha warsha, vikao, mijadala na mafunzo ya kujenga uwezo kwa wadau wa filamu
 • Kuhakiki picha jongevu na michezo yote ya kuigiza, kuipangia madaraja na kuitolea vibali
 • Kusimamia usambazaji na uoneshaji wa kazi za picha jongevu na michezo ya kuigiza
 • Kusimamia na kutoa leseni za uendeshaji katika sekta ya filamu pamoja na vitambulisho kwa wadau wa sekta hiyo. Leseni husika zinatolewa kwa majumba ya filamu na michezo ya kuigiza, wasambazaji, maktaba, studio, uanzishaji na uendeshaji wa matamasha na tuzo na utayarishaji wa kazi za picha jongevu
 • Kusimamia na kuratibu matamasha na tuzo za filamu na michezo ya kuigiza
 • Kusimamia utendaji wa Shirikisho la Filamu na vyama vya wadau wa sekta
 • Kutafuta fursa katika sekta na kuziwekeza kwa wadau
 • Kuratibu uibuaji vipaji kupitia michezo ya kuigiza na filamu
 • Majukumu mengine yoyote yanayohusiana na hayo