emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Utangulizi

Bodi ya Filamu Tanzania inawakaribisha watayarishaji wote wa filamu waje kutengeneza filamu zao katika mandhari adhimu na adimu. Moja ya majukumu yetu ni kutoa vibali vya utayarishaji wa filamu, kuwaunganisha watayarishaji wa filamu na mawakala wa kitanzania pamoja na mamlaka mbalimbali na taasisi za serikali, kushauri wadau kwa suala la raslimali zinazohusu upigaji wa picha /utengenezaji wa filamu Tanzania. Wakiwa Tanzania watafaidi mandhari nzuri, miji, wanyamapori, maliasili mbalimbali pamoja na tamaduni zaidi ya 140 zenye ukarimu na upendo.