emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Vibali vya Utengenezaji Filamu

Kwa Watayarishaji wa Ndani ya Nchi

Wahusika

Kampuni, taasisi au watu binafsi wa Kitanzania wanaotaka kurekodi picha jongevu kwa ajili ya kutayarisha filamu, makala za filamu, vipindi vya televisheni, matangazo na picha jongevu nyingine.

Taratibu za kupata kibali

1. Kujaza fomu ya maombi ambayo itaambatishwa na nyaraka mbalimbali ambazo ni:-

  • Barua ya kueleza nia ya kurekodi picha husika
  • Mswada wa filamu husika au synopsis)/story board kwa makala ya filamu na matangazo
  • Nakala ya kitambulisho cha mwombaji
  • Nakala za nyaraka za usajili wa kampuni husika
  • Uthibitisho wa hati ya malipo

2. Kuwasilisha ombi
3. Ombi kufanyiwa kazi
4. Kibali kutolewa baada ya ombi kuridhiwa


Ada: Kwa watanzania/filamu za kitanzania ni:

  • TZS. 50,000 (Utayarishaji filamu ya kwanza hadi ya Tano)
  • TZS. 500,000 (Mtayarishaji mwenye zaidi ya filamu Tano na filamu zilizofadhiliwa)
  • TZS. 2,000,000 (Utayarishaji wa matangazo ya Kibiashara)

(Bonyeza hapa kupakua fomu)