emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

BODI YA FILAMU NA SOMA INTERNATIONAL KUANZISHA MAHUSIANO YA PAMOJA NA TAASISI ZINAZOJIHUSISHA NA FILAMU PAMOJA NA MICHEZO YA KUIGIZA ZA NCHINI MAREKANI.


Jumatatu – Tarehe 16 Juni – 2025, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga amefanya mazungumzo na Mwanatasnia na Rais wa Taasisi ya Soma International Dkt. Mohamed J. Mwinyi ambaye amehitimu Shahada yaka ya Uzamivu kwenye masuala ya Sanaa, Utawala, Elimu na Siasa katika Chuo Kikuu cha Virginia Tech nchini Marekani.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Bodi ya Filamu zilizopo Kivukoni – Jijini Dar Es Salaam ambapo Bodi ya Filamu na Soma International wameazimia kuanzisha mahusiano ya pamoja na taasisi zinazojihusisha na Filamu pamoja na Michezo ya Kuigiza za nchini Marekani.

Azma kubwa ya kutengeneza mahusiano hayo imejikita katika kubadilishana ujuzi wanatasnia kimafunzo na kutanua wigo wa masoko ya kazi za filamu na michezo ya kuigiza nje ya mipaka ya Tanzania.