emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Uhakiki na Madaraja ya Filamu

Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 2011 zimeipa bodi hii mamlaka ya kuhakikisha inasimamia maudhui ya picha jongevu nchini Tanzania inayotangaza mila, desturi, urithi wa asili, kutangaza na kudumisha amani na utulivu.

Hivyo bodi imekabidhiwa mamlaka ya kuhakiki na kupangia madaraja filamu zote, video za muziki, vipindi vya televisheni, matangazo jongevu ya biashara, michezo ya video, vikaragosi jongevu, michezo ya kuigiza ya jukwaani pamoja na matangazo yake kabla ya kuoneshwa au kusambazwa kwa umma. Aidha, bodi imepewa mamlaka ya kutoa cheti cha uhakiki na alama ya madaraja kwa picha jongevu. (Bonyeza hapa kupakua fomu)


Madaraja ya Filamu

Filamu zinazohakikiwa na Bodi ya Filamu hupangiwa madaraja yafuatayo:


Alama ya Uhakiki

Alama ya Uhakiki inayotumika.

Muhimu: Hakuna picha jongevu au mchezo wa kuigiza utakaosambazwa au kuoneshwa kwa umma bila kuhakikiwa, kupangiwa madaraja, kupewa cheti pamoja na Alama ya Uhakiki.


Taratibu za Uhakiki na Ada zake

i. Kujaza fomu ya maombi,
ii. Kuwasilisha fomu hiyo bodi pamoja na nakala mbili za filamu husika na nakala mbili za matangazo (mabango) yake. Aidha, ataambatisha vibali vya kutumia maeneo, vifaa au maleba maalumu.


Ada

Muhimu: Malipo yote yatafanyika kwa kutumia namba ya malipo (control number) inayotolewa na Bodi ya Filamu.