emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

KATIBU MTENDAJI WA BODI YA FILAMU TANZANIA, DKT. GERVAS KASIGA AMEONGOZA KIKAO MAALUMU CHA SHAURI LA MWANATASNIA WA UCHESHI, BW. SHAFII HAMZA.


Jumatatu ya Tarehe 09 Juni, 2025—Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga ameongoza kikao maalumu cha shauri la Mwanatasnia wa Ucheshi, Bw. Shafii Hamza.

Shafii aliitikia wito wa Bodi ya Filamu Tanzania kusikiliza shauri lake kutokana na kuchapisha maudhui yasiyofaa kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Katika Kikao hicho, Bodi ya Filamu Tanzania imemuasa Mwanatasnia Shafii Hamza kuhakikisha anaitumia vizuri fani yake kwa kuzingatia maadili na tamaduni za Kitanzania. Bodi ya Filamu iimempa onyo kwa kuwa ni kosa lake la kwanza.

Shafii, amejutia kosa lake na amewaomba radhi Watanzania pamoja na mashabiki zake. Halikadhalika, ameahidi kutokurudia kosa la aina hiyo huku akisisitiza kuendelea kuwa balozi wa kuhamasisha uandaaji wa maudhui bora yenye tija kwa jamii.

Siku chache zilizopita, Bodi ya Filamu Tanzania ilimwelekeza Shafii kuondoa maudhui hayo mtandaoni na akatii. Bodi inazidi kutoa rai kwa Wanatasnia wote wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini kuendelea kufanya kazi zao kwa bidii ili waitangaze nchi yetu na wakati huo-huo wasiache kukumbatia maadili mema ya nchi yetu katika kazi zao.