emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Mandhari

Tanzania ni nchi nzuri, ambayo inaweza kupewa daraja la juu katika maeneo ya uandaaji wa filamu ndani ya Afrika. Nchi hii imejaliwa tamaduni mbalimbali za makabila yenye ukarimu kutoka pwani hadi bara na mapori. Mgawanyiko wa hali ya hewa kutoka mkoa mmoja hadi mwingine ni kivutio cha ziada kwa waandaaji wa filamu. Miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Arusha inawapa fursa waandaaji kukutana na zaidi ya tamaduni 130 kutoka mataifa mbalimbali yenye kuvutia, kitu ambacho kinafanya miji hiyo kukua kimataifa zaidi, yenye kukaribisha na kuvutia.


Mbali na uzuri huo: historia kubwa, fukwe za bahari, miji, vijiji na mapori, endapo utakuja kuandaa filamu ndani ya Tanzania utakuwa karibu sana na kilele cha Afrika. Tanzania ni nchi ya Kilimanjaro, kilele kirefu zaidi Afrika. Aidha, mbuga kubwa zaidi ya wanyama duniani Serengeti, iliyopewa jina na UNESCO kama hazina ya dunia, inahadithiwa kama ni nyumba ya misafara ya nyumbu ya mwisho wa mwaka ambayo ni kitu kinacholeta nakshi katika uandaaji wa filamu. Mbuga ya wanyama ya Serengeti ni maarufu kwa misafara ya nyumbu, kiasi cha milioni sita ya wanyama wakiwa nchi kavu, zaidi ya 200,000 pundamilia na 300,000 ya swala aina ya Thomson wanajumuika kwa pamoja kwa ajili ya kuota jua. Hata kama misafara ikiwa kimya, Serengeti inatoa nafasi nzuri kabisa ya kuandaa filamu Afrika: mikusanyiko mikubwa ya Nyati, makundi mdogo ya Tembo na Twiga, maelfu na maelfu ya ndege, Topi, Kongoni, Impala na Swala na Palahala.


Nchi ina mbuga za wanyama kubwa na nzuri kama Selous yenye kuvutia na maeneo mengi ya uandaaji wa filamu ya uhakika. Kituo kilipewa jina la raia wa Uingereza, Frederick Courtney Selous ambaye alikuwa ni mwanamazingira, mwindaji, mvumbuzi na mwandishi. Vitabu vyake vya mafunzo kuhusu Afrika vilivyokua na mauzo makubwa ndani ya Victorian, Uingereza.


Pia kuna kaldera za volkano kama kreta ya Ngorongoro ambacho ni kivutio kikubwa na maarufu duniani chenye mikusanyiko ya wanyama isiyo na uzio. Pia ni kituo kizuri ambacho mtu anaweza akaandaa filamu yake huku akivua samaki na kucheza michezo ya maji Afrika. Wote mnakaribishwa kuja kuandaa filamu katika maeneo mengine tofauti, pengine maeneo mazuri zaidi duniani kama mamia ya maili ya eneo la pwani ya bahari ya Hindi na maziwa yote makuu ya Afrika kama vile : ziwa Victoria, ziwa Tanganyika, na ziwa Nyasa (hakuna inchi yoyote inayokaribia zaidi hata ya moja ya maeneo haya).


Peruzi maeneo ya uandaaji wa filamu katika makundi yafuatayo:

Hifadhi na Mbuga za Taifa

Mbuga ya wanyama ya Arusha, mbuga ya wanyama ya bonde la Gombe, mbuga ya wanyama ya Katavi, mbuga ya wanyama ya Kilimanjaro, mbuga ya wanyama ya Kitulo, mbuga ya wanyama ya ziwa Manyara, mbuga ya wanyama ya Mikumi, mbuga ya wanyama ya Mkomazi, mbuga ya wanyawa ya Ruaha, mbuga ya wanyama ya kisiwa cha Rubondo na mbuga ya wanyama ya Serengeti.


Utalii anuwai

Utalii anuwai wa ndani ya bonde Gombe, mradi wa utalii ya Kilimanjaro, kituo cha nyoka cha Meserani, utalii wa milima ya Usambara na utalii wa milima ya Udzungwa.


Sehemu za Kihistoria na Mali Kale

Maandishi ya mapangoni ya Kondoa Irangi, mabaki ya Kaole, mabaki ya Isimila, mabaki ya Engaruka, Mikindani, eneo la hifadhi Ngorongoro, mapango ya Amboni, mabaki ya Kidichi Persian, hifadhi ya michoro ya mapangoni Kondoa, mapango ya Matumbi, makumbusho ya Mwalimu Nyerere, makumbusho ya Taifa ya Tanzania, makumbusho ya bonde la Olduvai, makumbusho ya Wasukuma, kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam, kisiwa cha Changuu (Prison Island), mabaki ya utumwa ya Mangapwani, mabaki ya kasri la Maruhubi, mabaki ya kasri la Mbweni, mabaki ya Mvuleni, Mji mkongwe Zanzibar, nyumba ya maajabu, mabaki ya ngome ya Kiarabu Bagamoyo na Zanzibar na kituo cha kihistoria cha Kalenga.


Chemchem za Maji Moto

Chemchem ya moto ya Chemka, Chemchem ya moto ya Maji moto Tanga, Chemchem ya moto ya Songwe na Chemchem ya moto ya Kikuletwa.


Maziwa

Ziwa Manyara, ziwa Natron, ziwa Nyasa, ziwa Tanganyika, ziwa Victoria, ziwa Eyasi na ziwa Empakai.


Misitu

Msitu wa Usambara mashariki, matunzo ya msitu wa Kimboza, eneo la mbao za Miombo ndani ya Tanzania, hifadhii ya msitu wa Mlinga na eneo tengefu la msitu wa Rondo.


Maporomoko ya maji

Maporomoko ya Rusumo, maporomoko ya Kalambo, maporomoko ya Soni, maporomoko ya Ndoro Marangu, maporomoko ya Sanje Tanzania, maporomoko ya Gibb’s Farm Karatu na mengine mengi.