Utengenezaji wa Filamu
Kampuni, taasisi, vikundi na watu binafsi wanaojihusisha na utengenezaji wa filamu na wanaohitaji kuja Tanzania kutengeneza filamu wanapaswa kujaza Fomu ya Maombi ya Upigaji Picha nchini. Wanatakiwa kuambatisha muhtasari wa filamu/makala, nakala za vibali vya kusafiri za kila mtu ambaye ataingia nchini kwa jukumu hilo, pamoja na orodha ya vifaa watakavyotumia ili kurahisisha masuala ya forodha. Waombaji wote wanashauriwa kuwasilisha fomu hiyo Bodi ya Filamu Tanzania angalau mwezi mmoja kabla ya kuanza shughuli za upigaji picha.