emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

ZIARA YA DKT. SERERA


Kufuatia uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Suleiman Serera, amefanya ziara kwa mara ya kwanza katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania kwa lengo la kufahamu namna Taasisi hiyo inavyofanya kazi.
Katika ziara hiyo Dkt. Serera amekutana na Menejimenti ya Bodi ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza menejimenti hiyo na kuitaka kuendelea kufanya kazi kwa bidii kulingana na mahitaji ya kisasa ili kuimarisha na kukuza Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.