emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

ZIARA YA BODI YA FILAMU


Katika kuendelea na utaratibu wa kutembelea wadau wake, Bodi ya Filamu Tanzania imefanya ziara kwenye ofisi za Uandaaji wa Filamu 'Kijiweni Productions' ambapo Katibu mtendaji Dkt. Kiagho Kilonzo amezungumza na Mkurugenzi wa Kijiweni Bw. Amir Shivji masuala mbalimbali ikiwemo mafanikio ya Makala yake mpya iitwayo 'KABURI WAZI' ambapo imezinduliwa Berlin nchini Ujerumani kwenye Tamasha la Filamu Berlinale na kutazamwa na watazamaji zaidi ya 800.

Pamoja na mambo mengine, Makala hiyo itaoneshwa katika majumba ya Sinema ya miji mitano tofauti nchini Ujerumani kuanzia mwezi Aprili 2024.