emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

HAPAWARDS KUFANYIKA TANZANIA


Taasisi za Bodi ya Filamu Tanzania pamoja Baraza la Sanaa la Taifa zimetangaza ujio wa Tuzo za Hapaward zinazotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza nchini tarehe 10 Agosti, 2024 katika ukumbi wa The Super Dom Masaki, jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu amesema Tuzo hizo zitatoa kipaumbele kwa Sekta ya Filamu ambapo zitakuwa na vipengele vya Filamu na wadau wa Filamu ili kutoa hamasa kubwa kwa Tasnia hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dkt. Kedmon Mapana amewashukuru waandaaji wa Tuzo hizo na kusema kuwa Baraza kwa kushirikiana na Bod ya Filamu litahakikisha linatoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha tukio hili linafanyika kwa ukubwa zaidi.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa HAPAwards Bi. Amberr Washington amesema kuwa wanayo furaha kufanya Tuzo hizi nchini Tanzania na anawakaribisha sana Wasanii na wadau kushiriki katika tuzo hizo.