emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

DULLVANI AOMBA RADHI


Kufuatia Msanii wa Maigizo Dullvani kupandisha mtandaoni maudhui yasiyokuwa na maadili katika jamii, Bodi ya Filamu Tanzania imemuita Msanii huyo kwa lengo la kumuelekeza namna sahihi ya kufanya kazi kwa kulinda maadili ya Kitanzania na kufuata Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976 na Kanuni zake za mwaka 2020.

Katika hatua nyingine Muigizaji Dullvani ameomba rambi kwa kosa alilofanya na ameahidi kutorudia kosa hilo. Aidha, ameahidi kuwa balozi wa kukemea maudhui yasiyofaa katika jamii.