Habari
KIKAO CHA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA FILAMU
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Mona Mwakalinga ameongoza Kikao cha tatu cha Bodi hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine kimefanya tathmini ya utekelezaji wa kazi za Bodi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na kutoa miongozo ya namna bora zaidi ya kutekeleza kazi hizo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wadau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.
Kikao hicho kimefanyika Juni 29, 2024 katika ofisi za Bodi, Kivukoni, jijini Dar es Salaam.