emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

BODI YA FILAMU KUSHIRIKIANA NA MEDEA


Taasisi za Bodi ya Filamu Tanzania na Media For Development and Advocacy 'MEDEA' zimekutana katika kikao cha awali cha kupanga namna sahihi ya kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya Sekta ya Filamu ikiwemo kuonesha Filamu katika maeneo ya wazi na matamasha, ambapo kwa kuanzia wanatarajia kuanza kuonesha Filamu kwenye Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalotarajiwa kufanyika Julai 2024 Mkoani Ruvuma.

Wa tatu kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Emmanuel Ndumukwa akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Bodi ya Filamu pamoja na MEDEA mara baada ya kikao hicho.