Habari
Waziri Pindi chana akutana na Kamati ya Haki za Wasanii

Katika kuendelea kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, tarehe 11 Agosti, 2023 Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwa mara ya kwanza amekutana na Kamati ya Haki za Wasanii kwa lengo la kufahamu namna inavyofanya kazi.
Kamati hiyo imekuwa ikiratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania tangu kuanzishwa kwake mwaka 2019.