Habari
WAZIRI PINDI CHANA AKARIBISHWA BODI YA FILAMU

Kufuatia uteuzi wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pindi Chana, tarehe 21 Februari, 2023 amefanya ziara kwa mara kwanza katika ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania kwa lengo la kuifahamu Taasisi hiyo na kuona namna inavyofanya kazi.
Katika ziara hiyo Mhe. Pindi Chana ameambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma, pamoja na Watendaji wengine kutoka Wizarani.