Habari
WAZIRI NDUMBARO AKABIDHI TUZO KWA JB NA PHINA

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi Tuzo za Hollywood and African Prestigious (HAPAwards) zilizofanyika hivi karibuni Hollywood Marekani kwa Muigizaji Jacob Stephene ‘JB‘ aliyeshinda kipengele cha "Best Bongo Movie Actor" na Mwanamuziki Saraphina Michael ‘Phina‘ aliyeshinda kipengele cha “Best Female in Bongo Flavor East Africa“ katika hafla maalum iliyofanyika Oktoba 17, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Waziri Ndumbaro ametoa rai kwa Wasanii nchini kuongeza ushindani wa kazi ili kuongeza tija katika uzalishaji, ubora na masoko ya kazi hizo hivyo itasaidia kuimarisha Sanaa kibiashara, uchumi na ajira.
Aidha, hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kaigho Kilonzo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa Dkt. Kedmon Mapana, watumishi kutoka kwenye Taasisi hizo, wadau wa Sekta ya Filamu na Muziki, pamoja na Waandishi wa Habari.