emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

WAZIRI MHE. DKT. DAMAS DANIEL NDUMBARO AKUTANA NA WAANDAAJI WA TUZO KUTOKA HOLLYWOOD MAREKANI


Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro leo Novemba 10, 2023 Jijini Dar Es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Tuzo za HAPAwards Bi. Tina Weisinger na Makamu wake Bi. Amberr Washington ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili juu ya Tanzania kuwa mwenyeji wa tuzo hizo msimu wa Nane mwaka 2024.

Mhe. Ndumbaro amewahakikishia viongozi hao kuwa Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji wa tuzo hizo ambazo zitasaidia kuongeza ubora wa kazi za Sanaa zinazozalishwa nchini.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo Pamoja na watendaji wengine wa Baraza la Sanaa la Taif na Bodi ya Filamu.

HAWAwards ni miongoni mwa tuzo kubwa za heshima zinazotolewa kwa wasanii wanaofanya vizuri nchini Marekani na Afrika ambapo kwa msimu huu wasanii wawili kutoka Tanzania Jacob Stephen (JB) na Saraphina Michael (Phina) walishinda tuzo hizo.