emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​WAZIRI MCHENGERWA ATEMBELEA STUDIO ZA WANENE KWA MARA YA KWANZA.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameambatana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo kutembelea Studio za Wanene Entertainment kwa lengo la kutazama uwekezaji uliofanywa na Kampuni hiyo.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Tarehe 13 Julai, 2022 Waziri Mchengerwa amejionea uwekezaji mkubwa ikiwemo Studio tatu za kisasa za kutayarisha Muziki na Filamu, ambapo alipata nafasi ya kutazama kazi mbalimbali zilizoandaliwa na Studio hiyo ikiwemo Filamu ya NYARA ambayo ni moja ya Filamu bora Barani Afrika.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mchengerwa amepongeza Kampuni ya Wanene Entertainment kwa uwekezaji huo kwakuwa unasaidia ukuzaji wa Sanaa nchini kupitia Muziki na Filamu kwa kuwapa nafasi vijana kuonesha vipaji vyao.

Aidha, amewataka Wanene kuendelea kufanya kazi bora zitakazotangaza Utamaduni wa Kitanzania na kuitangaza nchi yetu Kimataifa.