emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

WAZALISHAJI KUTOKA AUSTRALIA, USA NA TANZANIA KUSHIRIKIANA KUANDAA FILAMU YA ASANTE


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Mradi wa Filamu ya Asante amekutana na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo kupanga namna mradi huo utakavyotekelezwa.

Mradi wa Filamu ya Asante utashirikisha Waandaaji wa Filamu kutoka nchi za Tanzania, Marekani na Australia, ambapo pamoja na mambo mengine unalenga kuleta mapinduzi katika Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini katika maeneo ya Uandaaji wa Filamu kwa ubora, mafunzo na masoko ya Filamu kimataifa.

Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Bodi ya Filamu ambapo kimehudhuriwa na Katibu wa Kamati hiyo Profesa Martin Mhando, Mkurugenzi Msaidizi Haki na Maendeleo ya Wasanii kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Asha Salim, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Azam Media Limited Bw. Yahya Mohamed, pamoja na Afisa Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Bw. Samuel Kitalula.