emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

MAONESHO YA PICHA KITUO CHA UTAMADUNI


Katika kuendelea kudumisha uhusiano wa kimataifa na kidiplomasia baina ya Tanzania na Urusi kupitia Utamaduni na Sanaa katika Kituo cha Utamaduni wa Urusi, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga pamoja na ujumbe wake, wameshiriki hafla maalumu ya kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni na Sanaa cha Urusi Bw. Alexey Bondaruk na kumkaribisha Mkurugenzi mpya Bw. Alexander Evstigneev.

Hafla hiyo ilienda sambamba na uzinduzi wa maonesho ya kimataifa ya picha ya Andrei Stenin.