emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

UPIMAJI WA MARADHI YA MOYO KWA WASANII WA FILAMU


Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), pamoja na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeratibu kambi maalumu ya upimaji wa maradhi ya moyo kwa Wasanii wa Filamu na Sanaa zingine uliofanyika katika hospitali ya Moyo Jakaya Kikwete tawi la Mkapa Health Center lilipo Kawe jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Dkt. Peter Kisenge amesema kambi hiyo ya upimaji wa maradhi hayo imewezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo itafanyika kwa mwezi miezi miwili mfululizo katika siku za Jumamosi na Jumapili ikiwa na lengo la kusaidia wasanii kupima afya zao kabla ya kuathirika na magonjwa. Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza ari ya utendaji kazi. Aidha, ametoa rai kwa wasanii kujitokeza wingi katika zoezi hilo ili kupima afya na kusaidia kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Gervas Kasiga amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ufanyikaji wa vipimo vya maradhi ya moyo kwa Wasaniiya bila malipo. Isitoshe, amewataka wasanii kuwa mabalozi wazuri wa upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa kuwa wao ni vioo katika jamii hivyo kupitia hamasa yao, jamii itaongezeka ufahamu kuhusu magonjwa ya moyo.