emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

WASHINDI WA TUZO ZA FILAMU TANZANIA 2022 WAPATA MAFUNZO YA DIPLOMASIA


Katika kuendelea kuongeza weledi wa utendaji kwa wadau wa Filamu nchini, Bodi ya Filamu Tanzania imeratibu mafunzo ya THE COMING FILM STARS, kwa Washindi wa Tuzo za Filamu Tanzania 2022 ambapo mafunzo yamejikita katika masuala ya DIPLOMASIA.

Mafunzo hayo yametolewa Tarehe 22 Januari, 2023 na Mtaalam wa masuala ya Diplomasia Bi. Baikola Adam, katika maeneo yafuatayo:

1. Mavazi na muonekano mbele za Watu (Dress code);

2. Namna sahihi ya kuzungumza (Graceful conversations);

3. Kuheshimu watu (mutual respect);

4. Kuheshimu mialiko na utambulisho (etiquette in invitation);

5. Matumizi sahihi ya muda (punctuality);

6. Intelijensia ya kihisia ( emotional intelligence); na

7. Nidhamu ya michapalo (Dining etiquette and etiquette on formalities).