Habari
Wasanii wa kikundi cha Maigizo cha "King Jo Films"

Wasanii wa kikundi cha Maigizo cha "King Jo Films" kutoka Iyunga Mkoani Mbeya wakizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Emmanuel Ndumukwa, alipowatembelea katika eneo lao la kufanyia mazoezi ya Uigizaji tarehe 25 Mei, 2021.
Bodi ya Filamu imekuwa na utaratibu wa kuwatembelea Wadau wa Filamu katika maeneo ya kufanyia kazi ili kuona mazingira halisi ya utendaji wa Wadau wake, hivyo kugundua changamoto zilizopo na kuzitatua.