emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​WADAU WA SANAA WAANZA KUNUFAIKA NA MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa hundi za mamilioni ya fedha kwa wadau Sanaa waliokidhi kukopa kwenye mfuko wa Utamaduni na Sanaa na amewataka Wasanii na wadau wa kazi za Sanaa kujitokeza kwa wingi kuomba kukopeshwa fedha kutoka kwenye mfuko huo uliofufuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuwakwamua kiuchumi.

Hafla hiyo imefanyika Tarehe 23 Disemba, 2022 jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi rasmi wa utoaji mikopo kutoka kwenye mfuko huo.

Aidha, ofisi za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa zipo Kivukoni jijini Dar es Salaam katika majengo ya Utumishi karibu na ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Ofisi ya Hakimili Tanzania (COSOTA).