emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

Waandaaji na Waratibu wa HAPAwards WAFIKA TANZANIA


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo ameongoza kikao kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana, baina ya Menejimenti ya Baraza hilo pamoja na Waandaaji na Waratibu wa Tuzo za Kimataifa za Hollywood and African Prestigious (HAPAwards) za Hollywood, Marekani Bi. Tina Weisinger pamoja na Bi. Amberr Washington.

Kikao hicho kimefanyika Oktoba 9, 2023 katika ofisi za BASATA ambapo pamoja na mambo mengine kimelenga kujadili maandalizi ya awali ya namna Tanzania kuwa mwenyeji wa Tuzo hizo kwa mwaka 2024. Aidha, Waanzilishi hao wakiwa hapa nchini watakutana na Viongozi wa Wizara kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kupanua wigo wa Maendeleo ya Sekta ya Sanaa nchini.