emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

UZINDUZI WA TAMTHILIA YA EZRA


Kampuni ya Uandaaji wa Filamu na Tamthilia ya Lamata Villlage kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua Tamthilia mpya iitwayo EZRA katika ukumbi wa Century Cinemax Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umeudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo ambapo pamoja na mambo mengine, amepongeza uzinduzi wa Tamthilia hiyo kwani umeongeza fursa za ajira kwa washiriki na vilevile ameipongeza Vodacom kwa kuongeza wigo wa Soko la Filamu na Tamthilia nchini kupitia uzinduzi wa Televisheni mtandao ya Vodacom TV (VTV) ambayo itaanza kuonesha Tamthilia ya EZRA.