emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​UZINDUZI WA FILAMU YA THE GREEN TANZANITE


Tarehe 28/03/2023 Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya uandaaji wa Filamu ya Dar squad Tz imezindua Filamu ya THE GREEN TANZANITE yenye maudhui ya maisha ya Kitanzania.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Filamu kutoka Bodi ya Filamu Bw. Emmanuel Ndumukwa amepongeza waandaji wa Filamu wa Kampuni ya Dar Squad Tz kwa kuandaa kazi bora na yenye viwango vya Kimataifa.

"Sisi kama Serikali tunapongeza jitihada za Dar Squad Tz kwa kazi bora ambayo ina viwango vya kushindana na kazi za nje ya Nchi hivyo tunaamini itaweza kuitangaza Tanzania katika Tuzo za Kimataifa"

Kwa upande wake Muandaaji Mkuu wa Filamu hiyo Bw. Salman Bhamra amesema THE GREEN TANZANITE itaanza kuoneshwa kwenye kumbi za Sinema kuanzia tarehe 21/04/2023 Century Cinemax, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Aidha, ameeleza lengo la kuandaa Filamu hiyo ni kubadilisha utamaduni wa Watanzania kutazama Filamu katika kumbi za sinema kwa kuwa Filamu hiyo ina ubora na itaoneshwa kwenye kumbi za Sinema kwa mwezi mzima.