Habari
UZINDUZI WA FILAMU YA PIGO
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo aliemwakilisha Naibu Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma kuzindua Filamu iitwayo PIGO iliyoandaliwa na Muigizaji ambaye pia ni Muandaaji Bi. Mwahija Mungi.
Filamu hiyo yenye maudhui ya kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Saratani ya kizazi imezinduliwa Mkoani Mtwara katika Ukumbi wa Tiffany Diamond Hotel.


