Habari
UZINDUZI WA FILAMU

Pamoja na mambo mengine, Naibu Waziri ameupongeza mradi huo kwa kutumia Sanaa katika kutoa elimu kwa jamii hivyo anaamini kupitia Filamu hizo watu wengi watapata elimu kubwa kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Filamu hizo zimefadhiliwa na Mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na Virusi vya Ukimwi (PEPFAR), unaoratibiwa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
Aidha, Filamu hizo zimeandaliwa na Muandaaji na Muongozaji wa Filamu nchini Bi. Seko Shamte ambapo ameeleza kuwa zina lengo la kutoa elimu kwa jamii ya Kitanzania hivyo zitaoneshwa bila malipo yeyote katika majukwaa mbalimbali ikiwemo Televisheni ya Clouds ambapo tarehe 16 Machi 2023 itaoneshwa Filamu ya SWETA, tarehe 23 Machi, Filamu ya JASIRI na tarehe 30 Machi Filamu ya NIA.
Mkutano huo umehudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Bod ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo, Watendaji wa Bodi ya Filamu, wadau wa Filamu, pamoja na Waigizaji na Waogozaji wa Filamu zilizozinduliwa.