emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​UTAMBULISHO WA APPLIKESHENI YA SIMU LIVE


Katika kushirikiana na wadau wa Filamu, tarehe 26 Mei, 2023 Bodi ya Filamu Tanzania imeshiriki katika kutambulisha Applikesheni iitwayo SIMU LIVE kwa waandaaji wa Filamu nchini yenye lengo la kusambaza kazi hizo Kidijiti kupitia WWW.SIMULIVE.CO.TZ.

Applikesheni hiyo imeandaliwa na Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya Proin Promotions ambapo pamoja na mambo mengine, itasambaza maudhui mbalimbali kutoka Tanzania ikiwemo vipindi vya watoto, Makala, Vichekesho, vipindi Mbashara na Midahalo.