Habari
USHIRIKIANO BAINA YA BODI YA FILAMU TANZANIA NA UBALOZI WA UFARANSA

Bodi ya Filamu Tanzania imekutana na Maafisa wanaosimamia masuala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania na Ubalozi wa Ufaransa nchini Kenya na Somalia Bw. Etienne Pellausy pamoja na Bw. Serge-Armand Noukoue katika kikao cha kufahamu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Bodi.
Ziara ya Maafisa hao ni matokeo ya jitihada za Bodi ya Filamu kuanzisha ushirikiano wa kiutendaji baina ya Bodi na Ubalozi huo.