emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

UONESHAJI WA FILAMU MITAANI


Katika kujenga Utamaduni kwa Watanzania kupenda na kutazama Filamu za Kitanzania, Bodi ya Filamu Tanzania imeanzisha utaratibu wa kuonesha Filamu katika mitaa yao ili kuwafikia kwa karibu.

Tarehe 31/03/2023 Bodi imeonesha Filamu ya 'UGONJWA WA KIFO' katika viwanja vya Tabata Shule jijini Dar es Salaam. Filamu hiyo imeandaliwa na kampuni ya Tuyendage na kuongozwa na Muongozaji Juma Saada, ambapo ilifanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro cha Tuzo kubwa barani Afrika za Africa Magic Viewers Choice Awards kutoka nchini Nigeria.

Aidha, Bodi itakuwa ikionesha Filamu mitaani kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi.