emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​UFUNGUZI WA MAFUNZO YA KUANDAA MATAMASHA YA FILAMU


Bodi ya Filamu Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani (Goethe Institut), Taasisi ya A Wall is A Screen kutoka Ujerumani, pamoja na Asasi ya Ajabu Ajabu Audio Visual wamefungua rasmi mafunzo ya siku tatu (tarehe 14-16 Disemba) ya namna ya kuandaa matamasha ya kuonesha Filamu katika maeneo ya wazi kwa wadau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini.

Aidha, mafunzo yanafanyika katika ofisi za Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani (Goethe Institut) ambapo yatafungwa na utazamaji wa Filamu za Ujerumani na Tanzania, katika kuta za majengo ya kihistoria yaliyopo Kisutu jijini Dar es Salaam (Kuta ni Sinema) na baada ya hapo wataalamu kutoka Ujerumani, pamoja na washiriki wa mafunzo watahudhuria kilele cha Tuzo za Filamu Tanzania 2023 kitakachofanyika tarehe 16 Disemba, katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.