emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​TUZO ZA FILAMU TANZANIA 2022 ZAFUNGULIWA RASMI


Serikali kupitia Bodi ya Filamu Tanzania imefungua rasmi msimu wa II waTamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2022 ambapo Katibu Mtendaji wa Bodi wa Bodi hiyo Dkt. Kiagho Kilonzo ameeleza kuwa Tuzo hizo zinalenga kutambua mchango muhimu wa Wadau wa Filamu kupitia kazi wanazozifanya, kukuza vipaji, pamoja na kuchochea uandaaji wa kazi bora zitakazokuwa na ushindani ndani na nje ya Nchi.

Dkt. Kilonzo amesema kuwa, Serikali kupitia Bodi ya Filamu itahakikisha msimu wa II wa Tamasha la Tuzo za Filamu 2022 utakuwa bora zaidi ya msimu wa I hivyo wadau wa Filamu wachangamkie fursa ya uwepo wa Tuzo hizo.

Pamoja na mambo mengine, Katibu Mtendaji ameeleza kuwa tayari dirisha la kupokea Filamu zitakazoshiriki katika Tuzo hizo, limeshafunguliwa kuanzia Septemba 30, 2022 hadi Oktoba 30, 2022 ambapo kwa sasa Filamu zinaweza kuanza kuwasilishwa ofisi za Bodi ya Filamu, Kivukoni jijini Dar es Salaam, na kwa Filamu za mikoani utaratibu wa kuzipokea utatangazwa hivi karibuni.

Kauli mbiu ya Tamasha la Tuzo za Filamu 2022 ni "Filamu ni Biashara."