emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

TANZIA


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameungana na ndugu, Jamaa, marafiki, pamoja na wadau wa Filamu walioshiriki katika Sala Maalum ya mazishi ya Muigizaji mkongwe Bi. Chuma Suleiman almaarufu Bi. Hindu katika Msikiti wa Masjid Mwinyi Mkuu Magomeni jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo alimwakilisha Waziri Mchengerwa katika mazishi ya Muigizaji huyo yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mwinyi Mkuu Magomeni jijini Dar es Salaam.