Habari
TANZANIA NA UTURUKI KUSHIRIKIANA KATIKA MAFUNZO YA FILAMU
Katika kuendelea kuimarisha Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini, tarehe 7 Disemba, 2023 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo amekutana na Mratibu wa Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) Bi. Filiz SAHiNCi katika kikao cha kupanga namna sahihi ya ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Bodi ya Filamu na Serikali ya Uturuki kupitia Shirika hilo kwenye eneo la mafunzo ya uandishi wa miswada ya Filamu, uongozaji, uigizaji, uhariri, pamoja na upigaji picha za Filamu.
Aidha, mafunzo hayo yatatolewa kwa ushirikiano wa wataalamu na waandaaji wa Filamu kutoka Uturuki katika kipindi cha miaka mitatu ambapo kwa mwaka wa kwanza yanatarajiwa kufanyika Mei 2024 hapa Tanzania.