Habari
TAMASHA LA UTAMADUNI NA SANAA BAGAMOYO
Katika Tamasha la 43 la Kimataifa la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo, Bodi ya Filamu Tanzania imeonesha Filamu ya Nzowa iliyoandaliwa na Taasisi ya MEDEA yenye maudhui ya kufundisha jamii dhidi ya madhara ya ndoa za utotoni.
Kwa kuzingatia maudhui ya Filamu hiyo, Bodi imetoa kipaumbele kwa wazazi na watoto wa wilaya ya Bagamoyo ili waweze kujifunza na kuepuka kulazimisha watoto kuolewa kabla ya wakati.