emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

STAND UP COMEDIANS WAKUTANA BODI YA FILAMU


Katika kuendelea kuwafikia wadau wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini, tarehe 09 Oktoba, 2024 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo amekutana na wachekeshaji wa jukwaani maarufu kama STAND UP COMEDIANS, kwa lengo la kufahamiana nao na kuwapongeza kufuatia mwendo mzuri wa Tasnia hiyo.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Kilonzo amewashauri kuanzisha Chama rasmi kitakacho waunganisha na kuwatambulisha ili iwe rahisi kusikilizwa.

Sambamba na hayo, Dkt. Kilonzo amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo na kuepuka kubweteka kwa kutegemea Serikali kuwafanyia kila kitu. Aidha, amewaahidi Bodi kuendelea kuwapa ushirikiano wa asilimia 100 katika utendaji wa kazi zao.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wachekeshaji wa makundi mbalimbali wakiwemo @cheka.tu
@watubaki @tzpunchline