emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

RAIS SAMIA AFUNGA TAMASHA LA UTAMADUNI 2024


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Watanzania na wadau wa sekta ya Utamaduni na utalii kuona namna ya kuufanya utamaduni kuwa biashara ili ulete manufaa ya kiuchumi kwa nchi.

Ametoa rai hiyo wakati akihitimisha Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililofanyika wilayani Songea mkoani Ruvuma kuanzia Septemba 20 hadi 23, 2024 ambapo ametaja madhumuni ya matamasha ya utamaduni yanayofanyika nchini kuwa ni kuendeleza, kuenzi na kulinda tamaduni na mila za nchi pamoja na kufungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania kupitia kazi za sanaa na utamaduni.

Akizungumzia lugha ya Kiswahili, amesema kuwa haiwezekani nchi ikaongelea utamaduni bila kugusia lugha hiyo kwani ndiyo inayowaunganisha Watanzania na kuwafanya kuwa na utamaduni mmoja, pia imefungua fursa za kiuchumi kwa Watanzania na kutokana na hilo, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imejipanga kufungua vituo vya lugha ya Kiswahili 100 kwa kushirikiana na Diaspora kote duniani.

Akieleza kuhusu suala la mmomonyoko wa maadili, ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikia na taasisi na wadau mbalimbali kulifanyia kazi suala hilo na kuja na mapendekezo ya namna bora ya kulishughulikia.