emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​ONESHO LA HII NI AFRIKA MUSICAL THEATRE LAFANA


Katika kutekeleza Mpango Mkakati wa kurudisha Michezo ya Kuigiza jukwaani, Bodi ya Filamu imeunganana na Kundi liitwalo "Hii ni AFRIKA Musical Theatre" linaloongozwa na Bi. Abella Bateyunga, kuratibu onesho la mchezo wa jukwaani wenye maudhui ya muziki wa asili ya Kitanzania katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam tarehe 12 Agosti, 2023.

Dhima ya onesho hilo ni kuelezea Afrika ili dunia iweze kutambua kuhusu maisha ya Mwafrika na jamii zinazomzunguka hususan Mtanzania na makabila yake haswa kwenye upande wa ngoma, nyimbo, vyakula na maisha yao ya kila siku.

Mgeni rasmi katika onesho hilo ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb) ambapo aliambatana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania na Michezo ya Kuigiza Dkt. Kiagho Kilonzo.

Aidha, onesho hilo limehudhuriwa watu wengi wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali, pamoja na wadau wa Sanaa nchini.