emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​MUENDELEZO WA MAFUNZO KWA NJIA YA UCHAMBUZI WA FILAMU



Katika kuhakikisha Waandaaji wa Filamu nchini wanaandaa kazi zenye ubora na kuepuka makosa yanayojirudia mara kwa mara, Bodi ya Filamu Tanzania kupitia Wataalam wake imeendelea kutoa mafunzo kwa wadau wake kupitia uchambuzi wa Filamu ili kujadili kwa pamoja mapungufu yaliyopo na kuelekeza namna bora zaidi ya kutatua mapungufu na kuboresha kazi zijazo.

Tarehe 02 Agosti, 2022 Bodi imetoa mafunzo kwa Waandaji wa Filamu fupi iitwayo "KARANI" ambao ni Chama cha Waongozaji wa Filamu Tanzania (TAFIDA). Filamu hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wananchi kuhusu umuhimu wa zoezi la SENSA YA WATU NA MAKAZI, litakaloanza Tarehe 23 Agosti, 2022 nchi nzima.

Katika mafunzo hayo mapungufu kadhaa yalionekana na kuelekezwa namna bora ya kuboresha kabla kazi hiyo haijawafikia Watazamaji.