emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​MUENDELEZO WA KUTEMBELEA WADAU WA FILAMU WAKIWA KAZINI (LOCATION)Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo ameendelea na utaratibu wa kutembelea wadau wa Filamu kwa lengo la kuona mazingira halisi ya utendaji kazi.

Tarehe 19.09.2022 Dkt. Kilonzo amewatembelea Waandaaji wa Tamthilia ya HATIA, Magomeni jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo mengine amempongeza Muongozaji wa Tamthilia hiyo Bw. Jimmy Mafufu kwa kuwapa nafasi Waigizaji wengi wachanga kuonesha vipaji vyao.

Tamthilia hiyo inaoneshwa kupitia televisheni ya Sinema zetu, Jumatatu - Alhamisi, Saa 1 usiku.