emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​MTAA KWA MTAA MTWARA


Bodi ya Filamu Tanzania imeendelea na utaratibu wake wa kutembelea wadau wa Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza katika mitaa yao kwa lengo la kuona namna halisi ya utendaji wao.

Hivi karibuni Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Dkt. Kiagho Kilonzo aliambatana na Afisa Maendeleo ya Filamu Bw. Ally Makata kutembelea vikundi vya maigizo Mkoani Mtwara, ambapo walitembelea Kikundi cha Sanaa Mikindani kilichopo Mikindani na Kikundi cha Sanaa Tanzawood kilichopo Naliendele.