emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

​MMOJA WA WAASISI WA NOLLYWOOD ATETA NA BODI YA FILAMU


Katika kuendelea kufungua milango ya ushirikiano baina ya Bodi ya Filamu Tanzania na wadau wa Filamu wa Kimataifa, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Gervas Kasiga amefanya mazungumzo na mtayarishaji wa filamu na televisheni kutoka nchini Nigeria anayefanya kazi zake nchini Afrika Kusini ambaye pia ni mmoja ya waanzilishi wa Tasnia ya Filamu Nigeria (Nollywood) Bw. Faith Isiakpere. Faith ana tajriba pana ya kufanya kazi katika mashirika makubwa ya habari kama vile; BBC, BET, na Thames TV.

Mazungumzo hayo yamelenga masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Bodi hiyo na Mtayarishaji huyo katika kukuza na kuendeleza Sekta ya Filamu nchini ikiwemo eneo la mafunzo ya utayarishaji wa makala za video (Documentaries), pamoja na kuandaa matamasha ya filamu ya watoto yatakayowasaidia kufahamu na kuwatia kiu ya kupenda na kuthamini tamaduni za Afrika.