emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

MKUTANO MKUU WA DHARURA WA SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA (TAFF)


Kikosi Kazi hicho kilichojumuisha wajumbe kutoka kila Chama pamoja na Wanasheria kutoka Bodi ya Filamu na BASATA chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Kiagho Kilonzo, kiliandaa rasimu ya maboresho ya Katiba ya Shirikisho na Kanuni za Uchaguzi; na hatimaye kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa Shirikisho la Filamu tar 14 Machi, 2023 ambao umepitisha rasimu hizo. Aidha, baada ya Katiba hiyo kuidhinishwa na Mkutano Mkuu, sasa Shirikisho hilo litasajiliwa upya Bodi ya Filamu badala ya BASATA kwaajili ya kurahisisha huduma kwa Wanachama wake.

Baada ya zoezi hilo, Mkutano huo uliunda Kamati huru ya Uchaguzi iliyopendekeza Uchaguzi ufanyike tarehe 31 Machi, 2023.

Viongozi wa Kamati hiyo ni:
1. Mwenyekiti Bw. Michael Sangu,
2. Katibu Bw. Jumaa Baisar na

Wajumbe wafuatao:
1. Edwin Musiba;
2. Wilson Makubi;
3. Jerome Chitumbi;
3. Mariam Kakwaya;
4. Fadhili Mfate; na
5. Masoud Chumapesa.

Bodi ya Filamu itaendelea kusimamia masuala yote ya Filamu katika kipindi chote cha mpito hadi Uongozi mpya utakaposhika hatamu.