Habari
MAJADILIANO YA UWEKEZAJI KATIKA FILAMU

Katika kuendelea kufungua milango ya uwekezaji kwenye Sanaa hususan Sekta ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini, Taasisi za Bodi ya Filamu Tanzania na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) zimekutana na wawekezaji kutoka nchini India na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Sanaa.