emblem

Bodi ya Filamu Tanzania

Tanzania: Mandhari nzuri kwa Utayarishaji wa Filamu

Habari

MAFUNZO YA MIKOPO KWA WADAU WA SANAA NA UTAMADUNI


Katika kuelimisha Wadau wa Sanaa kuhusu Mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Bodi ya Filamu Tanzania imewakutanisha Viongozi wa Shirikisho la Filamu na Vyama vinavyounda Shirikisho hilo na Viongozi wa Mfuko ili kuwapa elimu Viongozi hao na kupokea Maoni ya namna ya kuboresha utoaji wa Mikopo.

Mafunzo hayo yametolewa na Afisa Utamaduni Mwandamizi Bi. Getrude Ndalo ambapo ameeleza kuwa, lengo la utoaji wa mikopo kwa Wadau wa Sanaa ni kuongeza ubora wa kazi zao ili zijiendeshe kibiashara na kuwa na ushindani wa Kimataifa.

Pamoja na mambo mengine, ameeleza kuwa mfuko unatoa aina tatu za mikopo ikiwemo mkopo wa kuendesha shughuli za Sanaa, mkopo wa kununua vifaa vya Sanaa, pamoja na mkopo wa kujikimu au dharura.

Aidha, zoezi la utoaji wa mikopo ni la muendelezo ambapo ofisi za Mfuko wa Utamaduni na Sanaa zipo Kivukoni kwenye majengo ya Utumishi karibu na ofisi za Bodi ya Filamu Tanzania.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Shirirkisho la Filamu Bw. Twiza Mbarouk, pamoja na Viongozi wa Vyama Nane kama ifuatavyo:-

1. Watayarishaji wa Filamu - TFPA

2. Waongozaji wa Filamu - TAFIDA

3. Wasambazaji wa Filamu - TAFDA

4. Watafuta Mandhari - TALOMA

5. Wahariri wa Filamu - TAFEA

6. Waalimu wa Filamu - TAMPTA

7. Waandishi wa miswada ya Filamu - TASA

8. Wapiga picha za Filamu - TCA